Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) yaingia makubaliano ya mauziano ya Mbolea Hai na TBPL ili kuimarisha upatikanaji wa Pembejeo Bora kwa Wakulima

Imewekwa: 10 June, 2026
Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) yaingia makubaliano ya mauziano ya Mbolea Hai na TBPL ili kuimarisha upatikanaji wa Pembejeo Bora kwa Wakulima

Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeingia makubaliano ya mauziano ya mbolea hai baina yake na Kampuni ya Tanzania Biotech Product Limited TBPL (Kampuni tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo -NDC) ambapo kampuni ya TBPL itakuwa ikizalisha mbolea hai kisha TFC kusambaza mbolea hizo kwa wakulima.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini hati ya mauziano ya mbolea hai kati ya NDC na TFC, iliyofanyika leo Mei 30, 2026, Kibaha, Pwani. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga ameeleza adhma ya Serikali ya kuhakikisha Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji wa pembejeo bora na salama za kilimo hususani mbolea hai zinazolenga kuongeza tija ya uzalishaji huku zikilinda mazingira na kutunza afya za watanzania.

Akimnukuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan juu kuimarisha kilimo chenye tija kupitia matumizi, sayansi na pembejeo bora zinazolinda afya ya udongo na mazingira. Mhe. Kapinga amesema makubaliano haya ni maono ya kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea uzalishaji endelevu.

Na kuongeza kuwa uzalishaji wa mbolea hai utapunguza gharama za matumizi ya fedha zinazotumika kuagiza pembejeo ikiwemo mbolea kutoka nje ya nchi na kuwezesha wakulima kupata bidhaa bora kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote ameeleza kuwa jukumu la msingi la TFC ni uagizaji, uzalishaji na usambazaji wa mbolea kwa wakulima nchini hivyo makubaliano haya ni muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata mbolea za aina zote kulingana na uhitaji wao.

Amesema kuwa makubaliano haya baina ya TPBL na TFC yanaonesha dhamira ya dhati katika kuongeza tija kwenye kilimo, kuboresha upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima na kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya kilimo inayokua kwa kasi.

slot gacor