Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na Kampuni tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo -NDC (TBPL) watia saini makubaliano ya Mauziano ya Mbolea Hai
Imewekwa: 10 June, 2026
Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeingia makubaliano ya mauziano ya Mbolea Hai na Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), Kampuni Tanzu ya NDC, ambapo TBPL itazalisha mbolea hai na TFC kusambaza kwa wakulima. Makubaliano hayo yanaunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha uzalishaji wa pembejeo bora za kilimo, kuongeza tija, kulinda mazingira na kuwezesha upatikanaji wa mbolea bora kwa gharama nafuu.

