Mtaalam wa BAGTECH kutoka Afrika Kusini awasili TFC kwa maandalizi ya Usimikaji wa Mtambo wa Kisasa wa kuchanganya Mbolea – Kurasini Dar Es Salaam
Imewekwa: 20 May, 2026
Mtaalam kutoka Kampuni ya BAGTECH ya nchini Afrika Kusini Fred Coelho (katikati), tarehe 19 Mei, 2026 amefika katika ofisi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TFC Bw. Samuel Mshote na Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara Bw. Lameck Borega kuhusu usimikaji wa mtambo wa kuchanganya mbolea (Fertilizer Blending Facilities).
Mtambo huo wa kuchanganya mbolea (Fertilizer Blending Facilities) unatarajiwa kufungwa katika eneo la Kurasini, jijini Dar es Salaam ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea.
Mtaalamu huyo amefika pia eneo linalokarabatiwa kwaajili kusimikwa mtambo na kutoa mapendekezo ya kitaalamu kisha kukagua makontena yaliyobeba vifaa vya mtambo huo.

