Ujumbe wa DRC watembelea Tanzania kuimarisha Ushirikiano wa kilimo
01 March, 2026 - 27 June, 2026
DAR ES SALAAM
barua@fertilizer.co.tz
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ulifanya ziara rasmi nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta ya kilimo. Ushirikiano huo ulilenga kuimarisha ushirikiano wa kiufundi, kuhamasisha uwekezaji katika minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo, na kukuza matumizi ya mbinu za kilimo endelevu na zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza tija, usalama wa chakula, na ukuaji wa uchumi.

