Accessibility Settings

Text Size

Color Contrast

Language

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Kilimo

Kampuni ya Mbolea Tanzania

/ News

Mkurugenzi Mkuu, Bw. Samuel Mshote aainisha nafasi ya TFC katika Mkutano wa Wabunge Wanawake (WPC) wa Jukwaa la Maziwa Makuu (FP-ICGRL) katika Maendeleo ya Kilimo.

Imewekwa: 15 May, 2026
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Samuel Mshote aainisha nafasi ya TFC katika Mkutano wa Wabunge Wanawake (WPC) wa Jukwaa la Maziwa Makuu (FP-ICGRL) katika Maendeleo ya Kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Bw. Samuel Mshote alipokuwa akieleza umuhimu wa TFC kama mdau wa Mkutano wa Wabunge Wanawake (WPC) wa Jukwaa la Maziwa Makuu (FP-ICGRL) utakofanyika Novemba 2026 jijini Dar es Salaam.

Kupitia fursa hii muhimu kwa TFC, Bw. Mshote ameeleza kuwa TFC inaunga mkono malengo ya mkutano huu hasa katika maeneo ya uwezeshaji wa kiuchumi, usalama wa chakula, maendeleo jumuishi, ushiriki wa wanawake na vijana, pamoja na ushirikiano wa kikanda. Kwa kuwa wanawake ni sehemu kubwa ya nguvu kazi katika sekta ya kilimo, upatikanaji wa mbolea bora unachangia moja kwa moja kuboresha maisha ya familia na jamii.

Kupitia shughuli za TFC za kuagiza, kuchanganya na kusambaza mbolea, TFC inalenga kuongeza uzalishaji wa kilimo, kuimarisha upatikanaji wa chakula, kusaidia wakulima wadogo hasa wanawake na vijana, pamoja na kuhamasisha kilimo endelevu na kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, TFC inaamini kuwa ushirikiano wa kikanda katika kilimo, biashara na maendeleo ya viwanda ni muhimu kwa amani na ustawi wa kiuchumi wa ukanda wa Maziwa Makuu. TFC iko tayari kuendelea kushirikiana na Mabunge, Washirika wa Maendeleo, Mashirika ya Wanawake na Sekta Binafsi katika kuendeleza mageuzi ya kilimo na usalama wa chakula.

slot gacor